KMPDU YADUMISHA UONGOZI WAKE
Madaktari nchini wamedumisha uongozi wa muungano wao KMPDU, baada ya kuwarejesha afisini kwa muhula mwingine viongozi wote wakuu wa muungano huo kupitia uchaguzi.
Kulingana na matokeo ya uchaguzi ulioandaliwa hapo jana, katibu Daktari davji Atella, amedumisha wadhifa wake bila kupingwa, huku naibu wake Daktari Dennis Miskellah akiibuka mshindi na asilimia 69 ya kura zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake Daktari Wendy Nyeera aliyepata asilimia 29.
Mwenyekiti wa kitaifa Daktari Abidan Mwachi, amedumisha wadhifa huo baada ya kumpiku Daktari Deogracious Maero na Daktari Benjamin Gikeri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































