#Local News

WANASIASA WAONYWA DHIDI YA UTEKAJI NYARA

Idara ya usalama nchini imewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuibua madai ya kutekwa nyara kwa lengo la kutaka kuhurumiwa na wapiga kura, ikisema wahusika watakabiliwa kulingana na sheria.

Onyo hii imetolewa baada ya Waziri wa zamani Raphael Tuju kujitokeza kutoka mafichoni, mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI, Mohammed Amin akikariri kwamba Tuju hakupewa hifadhi katika kaunti ya Kiambu, ila alikuwa chumbani kwake muda alioripotiwa kutoweka.

Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, amesema hulka hizo zitakomeshwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *