OMOLLO AONDOKA KCB KUELEKEA JAPAN
Klabu ya Raga ya KCB imethibitisha kuondoka kwa mchezaji chipukizi Andycolle Omollo ambaye anaelekea Japani kuanza masomo baada ya kupata ufadhili katika Chuo Kikuu cha Tenri.
Omollo, aliyejiunga na KCB akitokea MMUST, anatarajiwa kusafiri Jumamosi, Machi 28, hatua inayochukuliwa kuwa muhimu katika safari yake ya masomo na raga.
Mchezaji huyo ameonyesha kiwango cha juu katika msimu wa sasa wa Ligi ya Kenya Cup, akifunga majaribio sita na kutwaa tuzo za mchezaji bora katika mechi kadhaa, hali iliyomfanya kutambulika kama mmoja wa vipaji vinavyochipukia nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































