NAIYANOI NTUTU NG’ENO ATEULIWA KWENYE BODI YA ICTA
Naiyanoi Ntutu, mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr, Johana Ng’eno, ameteuliwa kuwa mjumbe wa wa bodi ya Mamlaka ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini.
Kupitia taarifa ya gazeti rasmi ya Aprili 2, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, William Kabogo, alimteua Naiyanoi kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwa taarifa hiyo.
Uteuzi huo unamweka katika nafasi muhimu ya kusaidia kuendeleza uchumi wa kidijitali na huduma za serikali mtandaoni, huku mwenyekiti wa ICTA, Lily Ng’ok, akikaribisha uteuzi huo na kuonyesha imani katika uwezo wake wa kuchangia kikamilifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































