VYUO VIKUU VYAMEZWA NA MADENI
Wizara ya elimu imelitaka bunge kuidhinisha bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 14.3 ili kuvinusuru vyuo vikuu vya umma nchini vinavyokabiliwa na hatari ya kufungwa kutokana na madeni ya zaidi ya shilingi bilioni 100.
Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu, katibu mkuu katika idara ya elimu ya juu Dakta Beatrice Inyangala, amesema kuna mapungufu ya shilingi bilioni 43.6 za HELB katika mwaka huu na ujao wa kifedha, ambayo yameweka hatarini mustakabbali wa maelfu ya wanafunzi.
Wizara hiyo sasa imetoa changamoto kwa vyuo vikuu kuongeza mapato yake ili kupunguza shinikizo la kifedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































