#Local News

MATIANG’I AKOSOA MATUMIZI YA FEDHA IKULU

Mwaniaji wa urais kupitia chama cha Jubilee Fred matiang’i, ameahidi kupunguza matumizi ya fedha za Ikulu kwa asilimia 80 iwapo wakenya watamchagua kuwa Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Akirejelea ripoti za mdhibiti wa bajeti ya serikali, Matiang’i amekosoa madai ya ubadhirifu wa fedha za umma katika Ikulu, akisema fedha zinazotengewa ikulu kwa sasa ni ukosefu wa utoaji kipaumbele kwa masuala yenye umuhimu.

Amepinga pendekezo la Ikulu kuongezewa mgao huku sekta muhimu zikidorora kutokana na uhaba wa fedha.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MATIANG’I AKOSOA MATUMIZI YA FEDHA IKULU

RUTO AANZA ZIARA MAGHARIBI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *