SIFUNA KUFAHAMU HATMA YAKE YA KUFURUSHWA LEO
Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, atafahamu hatima yake hii leo kuhusiana na kutimuliwa kutoka wadhifa huo, kwenye uamuzi ambao utatolewa leo na jopo la kushughulikia mizozo ya vyama vya kisiasa nchini.
Jopo hilo awali lilitoa agizo la kuzuia kwa muda utekelezaji wa uamuzi wa baraza kuu la ODM kumfurusha Sifuna kama katibu mkuu hadi wakati ambapo kesi ya Sifuna ingesikilizwa na kuamuliwa.
Kwenye uamuzi wa leo, Sifuna atabaini iwapo ataendelea kuhudumu kama katibu mkuu wa chama hicho au safari inatamatika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































