NYARIBO AITENGA SERIKALI YAKE NA MIILI 20 KERICHO
Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo, ameshinikiza uchunguzi kufanywa ili kubaini ilikotoka miili 20 ya ziada iliyofukuliwa kwenye kaburi la pamoja katika kaunti ya Kericho, akisisitiza kuwa serikali yake iliidhinisha miili 13 pekee kuzikwa kulingana amri ya mahakama.
Akizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu utata huo, Nyaribo amekariri kuwa utawala wake ulifuata taratibu hitajika katika kuizika miili hiyo, na kuwarushia lawama maafisa wanaosimamia makafani.
Maafisa 2 wa serikali yake wanazuiliwa na wapelelezi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































