MANYURU ATAKA USHIRIKIANO KUIMARISHA PVK
Mwenyekiti wa Pentecostal Voice of Kenya ambaye pia ni mchungaji wa Jesus Teaching Ministry, Apostle Peter Manyuru, amewataka wanachama wa muungano huo kushirikiana ili kuhakikisha ukuaji wa chama cha PVK.
Manyuru amesema ushirikiano huo utachangia kuimarisha wanachama, kuleta umoja na kuchochea ukuaji wa chama pamoja na makanisa yaliyo chini ya muungano huo.
Aidha, amewarai viongozi wa mashinani kuwa na mikakati ya kukuza huduma zao huku wakihakikisha ongezeko la wanachama kuanzia ngazi ya mashinani hadi kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































