RUTO ATETEA MPANGO WA SHA
Rais William Ruto amepuuza ukosoaji dhidi ya Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), akisema wanaoupinga hawana uwezo wa kuelewa mageuzi makubwa yanayoendelea katika sekta ya afya.
Akizungumza wakati wa mkutano na wanawake wa Maendeleo ya Wanawake, Rais ametetea mpango huo wa bima ya afya, akisema ni wa mageuzi na tayari unawanufaisha mamilioni ya Wakenya.
Ruto amewasuta baadhi ya viongozi kwa kusambaza taarifa potofu kuhusu mpango huo, akiyataja madai yao kuwa propaganda inayolenga kudhoofisha juhudi za serikali, na akapuuza kauli za wanaotabiri kuanguka kwa SHA kuwa hazina msingi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































