GEN Z WAHIMIZWA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA
Vijana wa kizazi cha Gen Z nchini wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kama wapiga kura ili kuafikia mageuzi ya uongozi wanayoshinikiza kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Akizungumza katika kaunti ya Kiambu, aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema hatua hiyo itawawezesha kuwatimua kutoka uongozini viongozi wanaoendeleza dhuluma dhidi ya vijana hao.
Alikuwa ameandamana na viongozi akiwemo mbunge wa Nyali Mohammed Ali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































