GAVANA LELELIT ATISHIA KUWASHTAKI MASENETA
Mvutano kati ya maseneta na magavana kuhusu uwajibika wa magavana umechukua mkondo tofauti, gavana wa Samburu Lati Lelelit akitishia kuwashtaki maseneta wanaohudumu kwenye kamati ya uhasibu wa fedha za kaunti kwa madai ya kumdhalilisha katika majengo ya bunge hapo jana.
Hii ni baada ya maseneta hao kujaribu kumkamata alipokuwa akiwahutubia wanahabari kwenye majengo hayo, siku kadhaa baada yake kupuuza maagizo ya kufika mbele ya kamati hiyo kutoa majibu ufujaji wa fedha za umma jinsi ilivyoibuliwa na mkaguzi wa hesabu za serikali.
Seneti sasa imesitisha hoja ya ugavi wa mapato ya kaunti iliyolenga kuongeza fedha kwa serikali hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































