RUTO AZURU NYANZA AKARIBISHWA NA ORENGO
Rais William Ruto amezuru kaunti za Siaya na Migori leo katika mwendelezo wa ziara yake eneo la Nyanza huku akikaribishwa na Gavana wa Siaya James Orengo hata baada ya mvutano wa kisiasa unaoshuhudiwa.
Rais anaendelea na mikutano yake na wananchi akielezea ajenda ya maendeleo katika maeneo hayo huku akiendelea kupigia debe miradi ya serikali yake akisisitiza umuhimu wa maendeleo kwa wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































