MWANGI ALENGA KIATU CHA DHAHABU NSL
Mshambuliaji wa Fortune Sacco, Collins Mwangi, ameweka malengo ya kumaliza msimu kama mfungaji bora katika Ligi ya Kitaifa huku akiendelea kung’ara mbele ya lango.
Kwa sasa Mwangi yuko nafasi ya pili akiwa na mabao 14, mabao matatu nyuma ya kinara Syphas Otieno mwenye mabao 17, huku Vincent Nyabuto akishika nafasi ya tatu kwa mabao 13. Zikiwa zimesalia mechi 13, ushindani wa tuzo ya mfungaji bora bado uko wazi.
Mwangi amesema mafanikio yake yanatokana na mshikamano na ushirikiano ndani ya kikosi cha Fortune Sacco, akitaja moja ya mechi bora alipofunga mabao manne katika ushindi mkubwa wa 9-0 dhidi ya Kabati Youth FC.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































