RUTO AONGOZA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NAIROBI
Rais William Ruto pamoja na Rais wa Msumbiji Daniel Chapo wameongoza kongamano la uwekezaji katika hoteli moja hapa jijini Nairobi.
Zaidi ya kampuni 20 zimekubali kuwekeza zaidi ya dola bilioni 2.9 katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo afya, kilimo na madini, huku kaunti kama Kilifi, Nairobi, Tana River na Kitui zikitajwa kunufaika.
Rais Ruto ametumia fursa hiyo kuwashukuru wawekezaji akisema Kenya iko tayari kwa uwekezaji, akiongeza kuwa raia wake wana uwezo na fursa bora za kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































