KWS YAKANUSHA UHARIBIFU WA MSITU NAIROBI
Shirika la Huduma za Wanyamapori limekanusha madai yanayosambaa mitandaoni kwamba linaharibu msitu wa nyanda za juu katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi.
Shirika hilo limesema madai hayo yanapotosha, likieleza kuwa kazi inayoendelea ni sehemu ya mpango halali wa kuhamisha kituo cha kulea wanyama yatima cha Nairobi.
Aidha, limesema hatua hiyo inalenga kuboresha uhifadhi wa wanyamapori, ustawi wa wanyama, huduma kwa wageni na elimu ya uhifadhi, likibainisha kuwa kituo cha sasa kilichoanzishwa mwaka 1964 hakikidhi viwango vya kisasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































