#Sports

KISUMU TAYARI KWA MICHEZO YA KSSSA

Jumla ya washiriki 3,600 wameratibiwa kushiriki michezo ya kitaifa ya shule za upili kwa muhula wa kwanza, itakayong’oa nanga tarehe 6 na kukamilika tarehe 12 mwezi huu katika kaunti ya Kisumu.

Kulingana na mkurugenzi wa masuala ya michezo katika wizara ya elimu Nelson Sifuna, ongezeko la idadi ya washiriki linaashiria matokeo ya mtaala wa umilisi CBC, ambao umeongeza idadi ya michezo shuleni.

Amesema hadi sasa kuna jumla ya michezo 25, idadi ya watakaoshiriki ikiongezeka kutoka 2,300 mwaka wa 2023 hadi 3,600 mwaka huu.

Naye katibu mkuu wa KSSSA David Ngugi, amethibitisha kuwa timu zitaanza kuwasili Jumapili hii kabla ya mashindano kuanza.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *