BONDIA OYOKO AFARIKI ULINGONI
Sekta ya ndondi nchini inaomboleza kufuatia kifo cha bondia Jacob Oyoko maarufu kama “Jack Spoiler”, aliyedondoka wakati wa pambano la kulipwa katika Ukumbi wa Utamaduni wa Mumias, Kaunti ya Kakamega.
Kifo hicho kilithibitishwa na rais wa Tume ya Ndondi za Kulipwa nchini, Reuben Ndolo, aliyesema bondia huyo wa Kisumu alifariki licha ya kupatiwa huduma ya dharura mara baada ya pambano. Tukio hilo lilikuwa sehemu ya hafla iliyoandaliwa na Rashid Echesa.
Ripoti za awali zinaonyesha Oyoko hakuweza kujilinda ipasavyo katika hatua za mwisho za pambano dhidi ya Julius Okuruchi, hali iliyozua mjadala kuhusu iwapo mwamuzi alipaswa kusitisha pambano mapema. Mamlaka husika zikiwemo polisi na wizara ya michezo zimearifiwa kuhusu tukio hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































