MVUTANO NDANI YA ODM WAZIDI KUTOKOTA
Naibu kinara wa ODM, Abdulswamad Sharif Nassir, amewataka viongozi wa mrengo wa Linda Mwananchi kusitisha mashambulizi ya maneno dhidi ya kinara wa chama hicho, Oburu Odinga, akisema wengi wa wanachama wanaunga mkono uongozi wake.
Akizungumza eneo la Jomvu wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara, Nassir amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya wengi ndani ya chama na kudumisha mshikamano wa kisiasa.
Aidha, amemtaka katibu wa chama, Edwin Sifuna, pamoja na wenzake kuwa na msimamo iwapo wanapanga kujiondoa chamani, akidai baadhi yao wanahusika na kubuni muundo wa chama. Vilevile ametetea viongozi wa ODM kutoka Pwani walioko serikalini kuhusu juhudi za kushughulikia ajira kwa vijana, masuala ya ardhi na usimamizi wa rasilimali za umma.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































