MAAFISA WA FKF WAPATA NYADHIFA NOC
Maafisa wanne wa Shirikisho la Soka nchini wamepata uteuzi katika Kamati ya Olimpiki ya Kenya, hatua inayotarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya uongozi wa soka na malengo ya michezo ya kimataifa.
Msimamizi wa timu ya taifa, Nick Kimanthi, ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa kiufundi, huku mwakilishi wa wanawake Violet Kerubo Momanyi akipewa jukumu la kuongoza kamati ya jinsia.
Wakati huo huo, mkurugenzi wa maendeleo ya soka Francis Kimanzi na afisa mkuu mtendaji Dennis Gicheru wameteuliwa katika kamati ya rufaa itakayoshughulikia masuala ya utawala, nidhamu na haki katika michezo
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































