METTE AFUNGUA USHINDANI KIKOSINI TUSKER FC
Kocha mkuu wa Tusker Julien Mette amesema hakuna mchezaji aliyehakikishiwa nafasi ya kuanza kikosini, akisisitiza kuwa uteuzi utafanywa kwa kuzingatia uwezo na juhudi za kila mmoja.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema msimamo huo tayari umechochea ushindani mzuri katika nafasi mbalimbali, hasa langoni ambapo ushindani umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Kipa mpya Pavelh Ndzila alivutia katika mechi yake ya kwanza kwa kutoruhusu bao lolote wakati Tusker ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kakamega Homeboyz mjini Mwea, hatua iliyoongeza ushindani na Brandon Obiero ambaye pia amekuwa akifanya vyema katika mechi za hivi karibuni.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































