KNCHR: FIDIA KWA WAATHIRIWA WA GHASIA ZA MAANDAMANO SI PESA PEKEE
Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu nchini imesisitiza kuwa mpango wa kutoa fidia kwa waathiriwa wa ghasia zilizotokana na maandamano unalenga kutambua makosa yaliyofanyika na kutoa haki, si malipo ya fedha pekee.
Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na wanahabari, mwenyekiti wa tume hiyo Claris Ogangah amesema fidia hiyo inapaswa kueleweka kwa upana na kujumuisha hatua mbalimbali zaidi ya malipo ya kifedha.
Ogangah ametoa wito kwa umma kuutazama mchakato huo wa fidia kama hatua muhimu kuelekea uwajibikaji na kutambua madhara yaliyowapata waathiriwa pamoja na familia zao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































