#Local News

KESI DHIDI YA MWALIMU ‘ALIYEMPA’ MWANAWE SUMU KUANZA APRILI

Mahakama kuu jijini Eldoret imepanga tarehe 21 mwezi ujao kuwa tarehe ya kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mwalimu mmoja wa shule ya msingi, Sylivia Bosibori, anayekabiliwa na tuhuma za kumwua mwanawe mvulana mwenye umri wa miaka 9 kwa kumpa sumu miaka 5 iliyopita.

Hakimu Emily Ominde ametoa agizo hilo baada ya upande wa mashtaka kuiarifu mahakama kwamba mshtakiwa alidinda kukubali makosa hayo kwa ajili ya suluhisho la nje ya mahakama, kesi hiyo ikiratibiwa kusikilizwa na hakimu tofauti baada ya Ominde kuiarifu mahakama kwamba amehamishiwa katika mahakama za Bungoma.

Bosibori anadaiwa kumwua mwanawe kati ya Mei 17 na 20 mwaka 2022 mtaani Joyland kutokana na ugomvi wa kinyumbani, na kisha kuendelea na shughuli zake za kufunza hadi majirani walipovutiwa na uvundo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *