PATEL ALENGA KUREJESHA UBINGWA WA AFRIKA KWENYE MBIO ZA MAGARI
Bingwa mara mbili wa mashindano ya magari ya mbio barani Afrika Karan Patel ameanza msimu wa mwaka 2026 kwa azma ya kurejesha taji la African Rally Championship.
Dereva huyo wa Kenya amesema ana dhamira ya kurejea kileleni baada ya kukosa ubingwa huo kwa karibu katika miaka ya hivi karibuni, akilenga kuthibitisha ubora wake katika mashindano ya bara.
Patel alianza kampeni yake kwa ushindi katika duru ya kwanza ya msimu, ikiwa ni mara ya kwanza kufanikisha hilo katika taaluma yake, hatua inayompa ari mpya na kuashiria nia yake ya kuwania ubingwa huo kwa dhati mwaka huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































