LAPORTA ACHAGULIWA TENA KAMA RAIS WA BARCELONA
Joan Laporta amechaguliwa tena kuwa rais wa Barcelona akimshinda Victor Font kuendelea kuiongoza miamba hiyo ya Catalan hadi 2031.
Mwanachama huyo mwenye umri wa miaka 63, ambaye pia alimshinda Font katika uchaguzi wa 2021, atarejelea wadhifa wake mwezi Julai baada ya kujiuzulu wiki chache zilizopita kama sehemu ya mchakato wa uchaguzi.
Karibu asilimia 42 ya wanachama wa klabu ya Barcelona walipiga kura na kufikia kura 48480. Laporta alishinda kwa asilimia 68.18 dhidi ya asilimia 29.78 ya Font.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































