MATUSI YA VIONGOZI YASHANGAZA TAIFA
Maswali yameibuka kuhusu ukiukaji wa sura ya 6 ya katiba kuhusu maadili miongoni mwa viongozi wakuu serikalini, kufuatia hatua ya viongozi hao akiwemo Rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua kurushiana matusi hadharani kuhusu mwonekano na masuala ya kibinafsi.
Wawaili hao wamekuwa wakirushiana matusi katika siku za hivi karibuni, wakenya wakijiuliza iwapo viongozi hao wana uwezo wa kuliendeleza taifa kimaendeleo na kimaadili, ukiwa umesalia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Akiwa kwenye ziara aliyoitaja kuwa ya maendeleo Magharibi mwa nchi hapo jana, Rais Ruto alirusha cheche za matusi, akijibu cheche sawa za za Gachagua ambazo hatuwezi kuzipeperusha kutokana na kanuni zetu za uhariri.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































