#Local News

MAHAKAMA YAONGEZA AMRI KUHUSU MCHAKATO WA KUMWONDOA DPP

Mahakama Kuu imeongeza muda wa amri ya kusitisha mchakato wa kuandaa kanuni za kumwondoa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.(DPP)

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mahakama kuthibitisha kuwa kesi inayotaka maafisa wa Tume ya Huduma za Umma kushtakiwa kwa kudharau mahakama ni ya dharura.

Mahakama imeagiza maombi yawasilishwe kwa wahusika wote ndani ya siku tatu, huku wakijibu ndani ya siku saba, na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 9 kwa maelekezo zaidi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *