BAO LA SSENYONJO LAWAPA INGWE USHINDI
AFC Leopards walifufua matumaini ya kuwania ubingwa wa taji la ligi kuu ya soka, KPL, kufutia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Nairobi United ugani Nyayo hapo jana.
Wakiwa na machungu ya kufungwa mabao 4-1 na Mathare United, Ingwe walirejea uwanjani humo kuwapa matumaini mashabiki na usimamizi wa klabu hiyo.
Bao ya majaribio na Subira, hatimaye mpenyo ulitokea katika dakika ya 38, Samuel Ssenyojo akifunga bao la pekee na kuwapa tulizo wana Ingwe.
Akizungumza baada mechi hiyo, kocha mkuu wa Ingwe Fred Ambani, alitaja ushindi huo kuwa ishara ya kuimarika baada ya kichapo wikendi iliyopita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































