DE LA FUENTE AKARIBISHA TETESI ZA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA
Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente, amesema anafurahia shinikizo la kuwa miongoni mwa wagombea wakuu wa kushinda Kombe la Dunia, akizungumza kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Misri jijini Barcelona.
De la Fuente amempongeza nyota, Lamine Yamal, huku akiepuka kusema iwapo ataanza mechi dhidi ya timu ya Misri, ambayo pia itashiriki Kombe la Dunia.
Timu hiyo, iliyopo nafasi ya kwanza katika viwango vya FIFA, iliibuka na ushindi wa 3–0 dhidi ya Serbia Ijumaa katika mechi ya kwanza ya kirafiki kati ya mbili zilizopangwa mwezi huu wa Machi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































