#Local News

UNAWEZA KUSAJILIWA KOKOTE, IEBC

Wakenya wanaolenga kusajiliwa kama wapiga kura wapya wana fursa ya kufanya hivyo katika eneo lolote waliko, na kuchagua kituo wanachopendelea kupiga kura.

Hii ni kulingana na tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, ambayo imeendelea kuwahimiza wakenya kujitokeza huku ikilenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni 2.5 ndani ya muda wa siku 30.

Zoezi hilo linaendeshwa katika wadi zote nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *