AMISI AKOSOA MATUMIZI YA VIJANA KUVURUGA MIKUTANO YA KISIASA
Mbunge wa Saboti Caleb Amisi amekosoa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaounga mkono serikali kwa madai ya kutumia vijana kuvuruga mikutano ya kisiasa ya upinzani.
Mbunge huyo amesema kuwa vitendo hivyo pia vinachochea utovu wa nidhamu miongoni mwa vijana na vinaathiri mazingira ya kisiasa yanayohitajika ili kuruhusu ushindani wa haki katika shughuli za kisiasa.
Aidha, Amisi amesema hatua hiyo inapunguza nafasi ya vyama vya upinzani kufanya shughuli zao kwa uhuru, akitoa wito kwa serikali kuwapatia vijana fursa za ajira badala ya kuwahusisha katika vitendo vya vurugu na machafuko.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































