#Local News

WAKENYA WAKATALIWA NA JESHI LA URUSI

Serikali ya Kenya italazimika kutafuta njia mbadala ya kuwarejesha nchini wakenya waliotia saini mkataba kupigana kwenye vita kati ya Urusi na Ukraine, baada ya Urusi kudinda kugharamia usafiri huo kwa misingi kwamba hakuna makubaliano ya kugharamia usafiri huo kwenye kandarasi zao.

Haya yamebainika baada ya mkutano wa faragha kati ya mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa masuala ya kigeni, na mwenzake wa Urusi Seregey Lavrov, ambaye amesema wakenya hao walijiunga na jeshi la Urusi kwa hiari.

Urusi imesema wakenya hawataruhusiwa tena kwenye jeshi lake huku waliomo wakianzisha mchakato wa kukatiza kandarasi zao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *