KENYA YATEKA MASOKO YA KIMATAIFA KUPITIA UZALISHAJI WA AINA MPYA YA MAUA
Kenya imeendelea kukumbatia aina mpya ya uzalishaji wa maua, hatua inayopanua zaidi masoko ya kimataifa kwa taifa hili linalochukua nafasi ya nne bora duniani katika uuzaji nje wa maua yaliyokatwa na ya mapambo.
Kulingana na ripoti ya Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Maua nchini Clement Tulezi, katika miaka ya hivi karibuni wakulima wa maua wameongeza uzalishaji wa maua aina ya waridi na mengine mapya yenye mvuto mkubwa kibiashara ngazi ya kimataifa.
Aina hizo mpya ni pamoja na spray roses, ambazo ni waridi za rangi mbalimbali zilizoboreshwa kwa muda wa kudumu kwenye chombo, hypericum inayotumika kama mapambo hasa kwenye harusi, maua aina ya baby’s breath, na limonium ambazo zinaongeza thamani sokoni kila kuchao.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































