TUSKER KWENYE JARIBIO JINGINE DHIDI YA POLICE
Klabu ya Tusker FC itarejea uwanjani hii leo baada ya kucharazwa na AFC Leopards bao 1-0 wikendi iliyopita, leo hii wakimenya na bingwa mtetezi Police FC katika mechi muhimu ya kusaka ubingwa wa taji la ligi kuu nchini, KPL.
Licha ya kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya Ingwe, Tusker walishindwa kufunga bao lolote na kupoteza pointi 3 muhimu.
Kocha mkuu Julien Mette, amekiri changamoto hiyo, akisema wamekuwa wakifanya kila wawezalo mazoezini kuimarisha makali yao.
katika mechi nyingine, Sofapaka wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja, watakabiliana na Bandari FC.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































