NTSA YATAKA KESI YA FAINI KUTUPILIWA MBALI
Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani, NTSA, imeiomba Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi inayopinga utekelezaji wa mfumo wa faini za papo hapo, ikisema suala hilo limepitwa na wakati.
Katika hati ya kujibu, mkurugenzi mkuu wa NTSA, Odhiambo Kondiwa, amesema mamlaka hiyo ilisitisha rasmi mpango huo Machi 27 mwaka huu hivyo kesi hiyo haina msingi wa kuendelea kusikilizwa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na kundi la Sheria Mtaani pamoja na wakili Shadrack Wambui waliokuwa wakipinga uhalali na utekelezaji wa mfumo huo wa faini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































