#Football #Sports

UBINGWA WA CAF: BERKANE, SUNDOWNS WATINGA NUSU FAINALI

Klabu za RS Berkane ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zilitinga awamu ya nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika katika mechi za mkondo wa pili wa robo fainali zilizokamilika hapo jana.

RS Berkane walihitaji muda wa ziada kufunga bao la ushindi, Mounir Chouiar akifuta makosa yake ya awali ya kupoteza penalti, na kufunga bao hilo muhimu kuipa Berkane ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Berkane ambao wanashiriki dimba hilo kwa mara ya kwanza baada ya kuibuka mabingwa wa dimba la mashirikisho msimu jana, walipata jumla ya mabao 2-1 kwenye mechi hiyo iliyochezwa nchini Rwanda.

Licha ya kichapo cha mabao 2-0 ugenini dhidi ya Stade Malien ya Mali, Sundowns walifuzu kwa wingi wa mabao, kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 katika mkondo wa kwanza.

Watamenyana Esperance ya Tunisia iliyowabandua mabingwa mara 12 Al Ahly ya Misri.

Na baada ya kuwashangaza mabingwa watetezi Pyramids na kuwabandua, AS FAR watamenyana na Berkane kwenye semi fainali nyingine.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *