SERIKALI KUTOA VITAMBULISHO KUANZIA SHULE YA UPILI
Katibu wa Idara ya Uhamiaji na Huduma za Wananchi, Belio Kipsang, ameongoza zoezi la kuwahamasisha machifu kuhusu mwongozo mpya wa kuwasajili Wakenya waliofikisha miaka 18 kupata vitambulisho vya kitaifa.
Zoezi hilo lililoanza mwezi Julai mwaka jana katika kaunti 20 limewezesha usajili wa watu milioni 1.7 hadi sasa, huku Kipsang akisema waombaji watapata vitambulisho ndani ya muda wa chini ya wiki moja.
Akizungumza Bomet, alisema mpango huo pia unalenga kuanzisha usajili shuleni kwa wanafunzi wa shule za upili kuanzia mwezi ujao ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































