#Local News

NDUNG’U ATAKA USAFISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Mwanaharakati Ndung’u Wainaina ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kusafisha daftari la wapiga kura wakati zoezi la usajili wa wapiga kura likiendelea kote nchini.

Wainaina, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Sera na Migogoro, amesema ukaguzi uliofanywa na KPMG kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ulibaini kasoro kadhaa katika sajili hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kulikuwa na nakala rudufu 481,711, wapiga kura 226,143 waliotumia vitambulisho visivyo vyao, rekodi 246,465 za watu waliofariki, pamoja na usajili 164,269 uliotumia nyaraka batili, hali inayozua haja ya marekebisho ya haraka.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *