ARSENAL YAPATA MOTISHA KABLA YA FAINALI DHIDI YA MAN CITY
Mshambuliaji wa Arsenal Leandro Trossard amesema ushindi wao kwenye UEFA Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen ni maandalizi bora kuelekea fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City.
Arsenal walifuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leverkusen, na kufanikisha ushindi wa jumla wa mabao 3-1, huku City wakiondolewa na Real Madrid katika mashindano hayo.
Sasa macho yanaelekezwa katika uwanja wa Wembley Stadium ambako vinara wa Ligi Kuu ya England Arsenal watakuwa wakisaka taji lao la kwanza msimu huu kwa kuilaza Manchester City, huku pia wakilenga kuweka historia ya kutwaa mataji manne.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































