FAMILIA YALALAMIKIA URITHI WA NDERITU GACHAGUA
Familia ya aliyekuwa Gavana wa Nyeri, James Nderitu Gachagua, imewasilisha ombi kwa Rais William Ruto ikitaka uchunguzi huru kufanyika kuhusu madai ya njama za kuwanyima urithi wao.
Kupitia barua iliyowasilishwa kwa Rais kupitia Mwanasheria Mkuu, familia hiyo inadai kuwa ndugu wa karibu aliingilia mchakato wa urithi kwa vitisho, hila na udanganyifu, hali iliyosababisha uhamishaji usio halali wa mali na hasara ya kifedha kwa warithi halali.
Mzozo huo unahusu waraka unaodaiwa kuwa wosia, ambao familia inasema si halali kwa kuwa umeandikwa “rasimu ya wosia wa mwisho,” jambo linalozua shaka kuhusu uhalali wake
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































