NATEMBEYA AONYA MADAKTARI WA UMMA WANAOPUUZA WAGONJWA
Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya amesema serikali yake haitavumilia madaktari walioajiriwa na umma wanaoshindwa kuwahudumia wagonjwa ipasavyo.
Natembeya ameeleza kuwa baadhi ya madaktari wanatumia muda mwingi kuendesha kliniki zao binafsi badala ya kutekeleza majukumu yao katika hospitali za serikali, hali inayodhoofisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Ameonya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika, akisisitiza kuwa kipaumbele cha serikali ya kaunti ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya katika vituo vya umma.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































