#Sports

UKAMILISHO WA TALANTA STADIUM WASUKUMWA MEI

Makataa ya kukamilishwa kwa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Talanta Sports City imesongeshwa kutoka Machi hadi Mei, uwezekano mkubwa ukiwa kwamba huenda ujenzi huo ukakamilika Julai mwaka huu.

Kuahirishwa huko kumejiri kufuatia ukaguzi wa kamati ya seneti kuhusu barabara, uchukuzi na miundombinu, inayosema imeridhishwa na hatua zilizopigwa hadi sasa.

Aidha, lengo lao la ukaguzi huo lilikuwa ni kubaini iwapo zabuni za ujenzi zilingatia sheria katika utoaji wake.

Mwanzoni mwa ujenzi, uwanja huo uliratibiwa kukamilika Desemba mwaka jana kabla ya kuahirishwa hadi Machi mwaka huu.

Kukamilika Julai kutaamanisha ujenzi huo umechelewa miezi 6 baada ya tarehe ya awali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *