HOSPITALI YA NAIROBI YAJITETEA KUHUSU HALI YA KIFEDHA
Hospitali ya Nairobi imetetea hali yake ya kifedha na uendeshaji wake ikisema huduma zinaendelea bila kukatizwa, huku ikilaumu mgogoro wa muda mrefu wa uongozi kwa taharuki iliyoshuhudiwa mahakamani na hadharani.
Katika mkutano na wanahabari, mwenyekiti wa bodi Barcley Onyambu pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji Felix Osano wamesema hospitali hiyo iko imara na inaendelea kutoa huduma kikamilifu bila kuathiri wagonjwa.
Maafisa wa hospitali hiyo pia wamepuuza takwimu zinazozunguka hadharani wakisema ni za kupotosha, wakikanusha madai ya kuwepo kwa upotevu wa shilingi bilioni 9.1, hasara ya bilioni 3 au mkopo wa bilioni 4.2 unaodaiwa kuchukuliwa na hospitali hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































