#Football #Sports

TUSKER YAJITOA MBIO ZA UBINGWA WA LIGI

Kocha mkuu wa Tusker FC, Julien Mette, amekiri kuwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu hazipo tena mikononi mwao, akiwataka wachezaji kuhamisha nguvu zao kwenye mashindano ya Kombe la FKF.

Timu hiyo, iliyotwaa ubingwa mara 13, itakabiliana na Kariobangi Sharks katika hatua ya 16 bora, huku ikiwa nafasi ya saba kwenye jedwali la ligi ikiwa na alama 37, nyuma ya vinara Gor Mahia kwa alama 19.

Mette amesema ni muhimu kukubali hali halisi na kuelekeza juhudi katika mashindano yanayoweza kuwaletea taji msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *