#Football #Sports

NOTTINGHAM, VILLA NA PALACE ROBO FAINALI ULAYA

Klabu ya Aston Villa itamenyana na Bologna katika robo fainali ya mashindano ya UROPA, baada ya kuandikisha ushindi wa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa jana usiku.

Mabao ya John McGin na Leon Bailey jana usiku yaliihakikishia ushindi Villa yake Unai Emery, na kuwapa nafasi katika awamu hiyo wanapolenga kurejea katika mashindano ya ligi ya mabingwa bara Ulaya.

Kwa upande mwingine, Nottingham Forest walikata tiketi ya kusakata dhidi ya Porto baada ya kuitandika Midjylland mabao 3-0 kupitia mikwaju ya penalty kufuatia sare ya mabao 2-2 licha ya Forest kupata ushindi wa mabao 2-1 katika muda wa ziada.

Katika mechi nyingine, Real Betis watachuana na Braga huku SC Freiburg wakimenyana na Celta Vigo.

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa tarehe 8 Aprili, isipokuwa Aston Villa na Bologna ambao watakutana tarehe 9.

Wakati uo huo, mabao mawili ya Ismaila Sarr yaliipa Crystal Palace ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya AEK Larnaca, na kuwapa Palace tiketi ya robo fainali katika mashindano ya Conference League. 

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *