MUDAVADI: HAKUNA FIDIA KWA WAATHIRIWA WA URUSI
Wakenya waliouawa au kujeruhiwa katika vita kati ya Urusi na Ukraine hawatapewa fidia na serikali, na badala yake serikali itawasaidia wanaotaka kurejea nchini kufanya hivyo.
Akizungumza jijini Moscow, Urusi, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amepuzilia mbali uwezekano wa serikali kuwapa fidia wakenya hao, akisisitiza msimamo wa Urusi kwamba walijitolea kupigana katika vita hivyo.
Familia za wakenya 10 waliouawa na mamia ya waliojeruhiwa zimekuwa zikiishinikiza serikali kuwajibika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































