#Local News

MBADI: BEI YA MAFUTA IMEPANDA KIMATAIFA

Waziri wa Hazina ya Taifa, John Mbadi, amesema serikali itaingilia kati kuwalinda Wakenya dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli katika soko la kimataifa.

Mbadi amesema serikali itatumia fedha kutoka kodi ya maendeleo ya mafuta, inayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 17, katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ili kupunguza shinikizo la bei kwa watumiaji.

Ameongeza kuwa serikali pia inazingatia marekebisho ya ushuru wa thamani (VAT) kwenye mafuta, licha ya kuwepo kwa akiba ya kutosha ya mafuta nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *