RISING STARLETS MBIONI KUFUZU FIFA U17
Timu ya taifa ya chipukizi ya wanawake, Rising Starlets, imeingia kambini kwa matayarisho ya mechi za kufuzu mashindano ya kombe la dunia kwa wachezaji wa umri usiozidi miaka 17, yaani FIFA World Cup U17.
Kenya itachuana na Namibia tarehe 12 mwezi ujao kwa mkondo wa kwanza nchini Namibia, kabla ya marudiano wiki moja baadaye jijini Nairobi.
Kocha mkuu wa Rising Starlets Mildred Cheche, amesema kikosi chake kimewajumuisha wachezaji wenye uzoefu, na wale wanaoinukia, akiongeza kuwa ana imani kuwa wachezaji hao wataisaidia Kenya kuafikia ndoto ya kufuzu kombe la dunia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































