VIFO VYA MAFURIKO VYAFIKIA 88
Idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini imefikia watu 88.
Kwa mujibu wa taarifa ya Huduma ya Polisi ambayo imetolewa hii leo, maelfu ya familia pia wameathiriwa huku miundombinu muhimu ikiharibiwa vibaya katika maeneo mbalimbali.
Zaidi ya familia 2,690 zimelazimika kuyahama makazi yao na kwa sasa zinaishi katika vituo vya muda huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika sehemu kadhaa za nchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































