#Football #Sports

ULINZI STARLETS WAKAZIA UBINGWA WA LIGI

Kocha wa Ulinzi Starlets, Collins Ochieng, amesisitiza kuwa timu yake ipo kwenye nafasi nzuri ya kushinda Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF msimu huu.

Ulinzi Starlets waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Trinity Starlets kwenye uwanja wa Comboni, Gilgil Jumapili, hatua iliyowainua hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 41, moja nyuma ya vinara na mabingwa wa awali, Kenya Police Bullets. Quinter Adhiambo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 48, huku Elizabeth Mideva akiongeza la pili dakika ya 69.

Vilevile, kwenye uwanja wa Mawego Polytechnic, Homa Bay, wenyeji Gideon Starlets waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Police Bullets kwa kupitia bao la Zaina Namuleme dakika ya 31. Ligi itaendelea Jumamosi huku Ulinzi Starlets wakikaribisha Vihiga Queens na Police Bullets kukutana na Kibera Soccer Women katika uwanja wa Police Sacco.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *